Knowledge

FAHAMU MAANA YA SHEMASI, AINA ZAKE NA WAJIBU WAKE NDANI YA KANISA KATOLIKI.

Shemasi ni neno la Kiarabu, ambalo kwa Kigiriki ni ".." yaani "Diakonos" Maana yake ni Mtumishi, Msaidizi, Mhudumu au Mjumbe. Pia ni Kiongozi wa Kanisa anayewaunganisha wenye Daraja za juu na Walei.
Shemasi ni cheo au daraja la tatu na la chini zaidi katika Sakramenti ya Daraja Takatifu. Maana Daraja Takatifu linaundwa na hatua tatu: Ushemasi, Upadre na hatimaye Uaskofu.
Lakini katika Kanisa la Moravian, Ushemasi ni ngazi ya kwanza kabisa katika Uchangaji.
Hivyo Kanisa Katoliki linasimamia na baada ya mchakato wa Mkatoliki Mbatizwa kupitia elimu ya Degree za Falsafa na Teolojia, na baadaye kuwekewa mikono na Askofu.
Katika cheo hiki, Shemasi anahesabika kama Mkleri, anayeshikia nafasi ya Wakleri kwa mikono aliyowekewa na Askofu, naye kwa pamoja anashiriki Daraja Takatifu kama ilivyo kwa Mapadre na Maaskofu wengine.
Swali: Ushemasi ulianza lini?
Jibu: Ushemasi katika Biblia ulianzishwa kwenye Agano Jipya hasa zaidi baada ya Mitume kuweka Viongozi saba ili wawasaidie katika kuliongoza vema Kanisa la Yerusalemu, miongoni mwao alikuwa Mtakatifu Stephano Shahidi. (1Timotheo 3:1-13)
Swali: Kuna aina ngapi za Ushemasi? Jibu: Katika Kanisa Katoliki kuna aina kuu mbili za Ushemasi, nazo ni:-
1. Mashemasi wa mpito.
Hawa ni wale Mashemasi tuliowazoea baada ya kupewa Daraja la Ushemasi, hukaa kitambo kidogo takribani miezi sita au zaidi huku wakifanya kazi za Uchungaji na baadaye kupadrishwa.
2. Mashemasi wa kudumu.
Hawa ni Mashemasi wanaoshika Daraja hilo la Ushemasi pasipo na muelekeo au nia ya kupadrishwa.
Shemasi wa aina hii anaweza kuwa Mwanadoa au la, kutegemea na kipindi gani cha Daraja hilo la Ushemasi aliopewa. Kwani endapo atakuwa hajaoa, basi atadumu bila ndoa katika Daraja lake hilo la Ushemasi hadi kufa.
Swali: Majukumu ya Shemasi ni yapi?
Jibu: Majukumu ya Shemasi ni kubatiza, kushuhudia ndoa, kuzika baada ya Misa ya mazishi kuisha, kukomunisha, kuhubiri Injili au homilia na kusali sala za Kanisa.
Hivyo tuendelee kuwaombea Mashemasi wetu popote walipo, ili wawe mfano bora wa Kristo na Mungu awajalie nguvu katika utume wao.
Tumsifu Yesu Kristo!

"During these 40 days, let me put away all my pride. Let me change my heart and give up all that is not good within me. Let me love God with all that I am and all that I have." —Genesis Grain.