Knowledge

NINI MAANA YA "IHS".

Wengi tumekuwa tukishangaa mavazi ya mapadre, vitambaa na vitu mbalimbali vya ibada kuwa na alama hiyo (kama kwenye picha hapo). Leo nataka nikujuze maana yake na historia yake. (jitahidi usome mpaka mwisho)
Maneno yasiwe mengi. "IHS" ni ufupisho wa jina Takatifu la Yesu kwa Kigiriki IHEOYE. Na imeanza kutumika tangu karne ya pili hata leo karne ya 21.
Hapo kabla kipindi wakristu wakiteswa na kuuawa na utawala dhalimu wa Kirumi, ilitumiwa kama alama ya siri (secret code), ilikua ikiandikwa katika nyumba, kaburi, na makanisa ya siri ya wakristu (nao wakristu wakiiona wanajua hapo ndipo kwao)
Mt. Bernardine wa Siena (1380-1444) na mwanafunzi wake, Mt. Yohana wa Capistrano (1386-1456) waliitumia alama hii kueneza ibada kwa Jina Takatifu la Yesu katika maeneo mbalimbali huko Italia, na miujiza mingi sana ilitendeka. Watu wakaanza kuhisi ni ushirikina. Ndipo Papa Martin V mnamo mwaka 1427 aliopitisha ibada hii na akaelekeza iwekwe pia msalaba katikati yake (kama kwenye hilo vazi pichani).
Watu wanashangaa inawezekanaje jina kuponya? Yesu mwenyewe aliahidi hili. "Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.” (MARKO 16: 17-18). Soma pia: Mdo 2:21, Mt 4:1-11, Yoh 16:23-24, Kol 3:17.
Lakini pia kutokana na kufifia kwa matumizi ya kigiriki na kutawala kwa kilatini enzi hizo, alama hiyo ya IHS iliweza pia kutafsiriwa kwa namna nyingine bila kuharibu maana. IHS = Iesus Hominum Salvator (ikimaanisha Yesu Mwokozi wa Wanadamu)
Kikubwa, alama hiyo ipo kwa ajili ya kutangaza ukuu wa Jina Takatifu la Yesu.

"During these 40 days, let me put away all my pride. Let me change my heart and give up all that is not good within me. Let me love God with all that I am and all that I have." —Genesis Grain.