Knowledge

KUFUNIKWA KWA SANAMU NA MISALABA KUANZIA DOMINICA YA 5 YA KWARESMA.

Misalaba na sanam hufunikwa kabla ya masifu ya jioni ya jumamos inayotangulia Jumapil ya tano ya Kwaresma. Misalaba hufunuliwa tu mara baada ya Ibada ya Mateso siku ya Ijumaa kuu, na sanam hufunuliwa siku ya jumamos mwanzo wa adhimisho la mkesha wa Pasaka ( Wakati wa Utukufu).
Kwanini sanam na nisalaba hufunikwa? Zipo sababu kuu mbiki, moja ya kibiblia na nyingine ni ya Kimantiki(Logic) na Kitiolojia.
1. Kuna matukio makubwa mawili Yesu alilazimika kujificha, a) Yesu aliwaambia wayahudi kuwa, "Kabla Abrahamu hajazaliwa yeye alikuwepo" wayahudi waliokota mawe ili wamtupie lakini Yesu alijificha, akatoka hekaluni. Rejea YOHANE 8:58-59.
b)Wayahudi walimwamini Yesu baada ya kunfufua lazaro. Hata hivyo, makuhani wakuu na Mafarisayo walianza kumtafuta Yesu ili wamuue kwani walimwona ni tishio kwa Dini yao na Taifa kwa ujumla. Yesu alipojua mipango yao, hakutembea tena hadharan kati ya wayahudi, bali alitoka hapo akaenda mahali Karibu na jangwa. Rejea YOHANE 11:54. Hivyo, tendo la kufunika Misalaba linatukumbusha kuwa, "Yesu mwenyewe alianza kujificha na hivyo, kutokuonekana kwa kuwa alijua saa yake ya kutukuzwa bado.
2. Sababu ya pili ni ya Kimantiki na Kiteolojia. Kipindi cha kwaresma tunatafakari nateso ya Bwana. Katika kipindi chote cha Mateso na kifo chake Kristo, alificha Umungu wake, na hivyo kuonekana kama binadamu wa kawaida asiye na nguvu yeyote. Hivyo, kitendo cha kufunika sanamu na Misalaba kinaashiria pia Yesu kuficha/Kufunika Umungu/Utukufu wake na kuonekana katika hali ya kibinadamu zaidi.
Swali Jepesi. Je! Kwanini sanam nyingine za Watakatifu pia hufunikwa? Jibu ni Rahisi. Haifai Watumishi kujionyesha hadharani wakati Bwana wao amejificha. (It is Improper for the servant to show themselves when the master is hidden).
Tumsifu Yesu Kristu

"During these 40 days, let me put away all my pride. Let me change my heart and give up all that is not good within me. Let me love God with all that I am and all that I have." —Genesis Grain.